Shule za msingi nchini Uingereza zinatarajiwa kufunguliwa Juni 1, 2020 baada ya kufungwa kwa muda kama hatua ya kudhibiti kusambaa kwa virusi vipya vya corona (covid-19).
Waziri Mkuu, Boris Johnson amewataka wazazi wa wanafunzi wa shule za msingi kuwaandaa kurudi shuleni. Shule zote zilifungwa Machi 20, 2020.
Maamuzi hayo ya kufungua shule ni ya Uingereza pekee. Scotland watafungua Agosti 11 na Ireland Kaskazini wanatarajia kufungua Mwezi Septemba.
Wasafiri kutoka Brazil marufuku kuingia Marekani
Boris amesisitiza kufungua shule za msingi japo shule nyingine hazitafunguliwa kwa kuwa vyama vya waalimu na wazazi bado hawana uhakika wa usalama kwa kipindi hiki cha janga la virusi vya Corona.
Uingereza ina jumla ya visa 259,559 na vifo 28,752 vya covid 19
Madareva wa malori 200 wapimwa Corona Dar, Ummy awapa ushauri