Serikali ya India imetangaza kurejesha safari za ndege za ndani kuanzia leo, Mei 25, 2020 licha ya kuongezeka kwa visa vya maambukizi ya virusi vya corona, huku abiria wakiingiwa na mashaka kuhusu sheria za kukaa karantini.

Machi mwaka huu, nchi hiyo ilisitisha safari zote za ndani ya nchi na kimataifa kama hatua ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.

Kurejea kwa safari hizo za ndege baada ya miezi miwili kumeanza na changamoto ya aina yake ambako kati ya ndege 380 zilizotarajiwa kufanya safari zake leo, ndege 82 zimeahirisha safari zake; na ndege 20 zimefuta ratiba ya safari katika jiji la Bengaluru.

Ndani ya kipindi cha siku mbili tangu nchi hiyo iruhusu ndege kutoka nje kuingia, jiji la Kerala limeripoti zaidi ya visa vipya 50 hadi jana, ambapo watu wengi waliorejea kutoka nchi za nje wamekutwa na maambukizi.

Imeelezwa kuwa kati yao walioathirika, wapo ambao waliingia kupitia program ya Serikali ya kuwatoa raia wake katika mataifa mbalimbali.

Jiji la Kerala hivi sasa limethibitisha kuwa na visa vipya 847, huku 322 wakiwa wanaishi na virusi vya corona. Takwimu hizi ni kuanzia Mei 10, 2020 ilipoanza program ya kuwarejesha raia wake kutoka nchi za nje.

Uingereza: shule za msingi kufunguliwa juni 1

Madareva wa malori 200 wapimwa Corona Dar, Ummy awapa ushauri

Wataalam Uingereza: Corona inapotea kwa kasi, matumaini mapya kupata dawa
Shule za msingi kufunguliwa Juni 1 - Uingereza