Waziri wa Nishati, January Makamba amesema wanaridhishwa na kasi ya Ujazaji maji Bwawa la kuzalisha Umeme la Mwalimu Nyerere Hydro Power na kwa sasa limefikia ujazo wa lita za Maji Bilioni Sita huku kukiwa kumebaki na mita kumi na tatu kufikia Kiwango cha Maji yatakayoweza kuzungusha mitambo hiyo ya kufua Umeme.
Makamba ameyasema hayo mara baada ya kutembelea mradi huo wa kufua umeme akilenga kujinea maendeleo yake kwa akuambatana na Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini – TANESCO, Maharage Chande.
Amesema kiwango hiko ni kizuri kutokana na kuzidi matarajio yaliyokuwepo awali wa uzinduzi wa ujazaji maji uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan na kwamba maendeleo yake yanaridhisha ingawa kazi bado ipo ya umaliziaji wa matengenezo ya Bwawa hilo.
Kwa mujibu wa takwimu kwa wiki mbili zilizopita kiwango cha uingiaji maji maji yameingia mengi kuliko yaliyoleta mafuriko 2019/2020, neema iliyopo zile athari za mafuriko hazipo tena. Bwawa hili limeanza kuzaa matunda tuliyotarajia ikiwemo kudhibiti mafuriko kwa sasa tuko asimilia 86 wakati Rais Samia anachukua madaraka ya nchi mradi huu ulikua ni asilimia 37.