Ujenzi wa Reli ya kisasa SGR kwa kipande cha kwanza kati ya Dar es Salaam hadi Morogoro chenye kilomita 300 umefikia asilimia 87 huku sh trilioni 1.7 zikiwa zimeshalipwa hadi sasa.
Mkurugenzi wa Mkuu wa Shirika la Reli TRC Masanja Kadosa amesema uwekaji matuta umefikia asilimia 91 wakati madaraja na makaravati yakiwa yamefikia asilimia 90, ameyasema hayo Akizungumza Wakati Baraza la Uongozi Chuo cha Taifa Usafirishaji NIT lilipotembelea mradi huo, Agosti m14 2020,
“Hali ya hewa na na ardhi ndiyo changamoto kubwa zinazotusumbua katika mradi huu, kuna wakati mradi ulisimama kwa muda kwa sababu mvua zilikuwa kubwa sana, lakini hivi sasa kazi inaendelea vizuri.” Amesema Kadogosa.
Ameongeza kuwa ziara ya NIT ina umuhimu mkubwa kwani bila kuwa na rasilimali watu ya kutosha miradi mingi inayoendelea sasa inaeza kushindwa kuendelezwa.
Naye msimamizi wa ujenzi wa mahandaki katika eneo la kilosa Injinia Amir Hamis amesema kazi inaendelea kwa kasi na kwamba mahandaki yote manne yako katika hatua za mwisho za ujenzi.
kwa upande wake mkuu wa NIT Profesa Zacharia Mganilwa amesema ziara hiyo ilikuwa na lengo la kujifunza na kuangalia namna wanavyoweza kuandaa rasilimali watu kwa sekta muhimu kama ya reli.
Kipande cha ujenzi wa SGR Dar- Moro chenye kilomita 300 kilianza kujengwa Mei 2, 2017 na hadi kukamilika kwake kiyaghariku zaidi zaidi ya sh trilioni 2.