Wanasiasa wa upinzani nchini Kenya, wamesisitiza kuendelea na maandamano ya kitaifa Yatakayo hitimishwa siku ya Jumatatu ijayo (Machi 20, 2023), jijini Nairobi ambayo yanalenga kufikisha ujumbe wao wakilalamikia kupanda kwa gharama za maisha.
Kiongozi wa upinzani wa Chama cha Orange Democratic Movement – ODM, Raila Odinga ameitangaza tarehe hiyo kuwa siku ya mapumziko, ili wakenya waweze kushiriki kwenye maandamano hayo tamko ambalo limezua mitazamo tofauti, kwakua si la kisheria.
Naibu Gavana wa Kaunti ya Kisumu, Mathew Owiti amesema maandamano hayo yanatoa maandalizi ya siku mbili, ili kuitikia wito wa Odinga, huku waandamanaji wakikusanyika mjini Kisumu ambako wameahidi kukutana tena siku ya Ijumaa kujiandaa na kilele cha hoja zao.
Hata hivyo, Kiongozi wa chama cha NARC – Kenya, ambacho ni sehemu ya muungano wa Azimio, Martha Karua amesisitiza kuwa dawa ya kutafuta suluhu ya nafuu ya kimaisha ni kutumia njia ya
maandamano ya amani, ili kudai haki kwa wakenya.