Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasili Jijini Pretoria nchini Afrika ya Kusini, kwa ajili ya ziara ya Kiserikali ya siku moja akiwa ameambatana na ujumbe wake akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Waterkloof Air Force Base Pretoria kwa ajili ya kuanza ziara rasmi ya Kiserikali nchini Afrika Kusini tarehe 15 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya Maua kutoka kwa Mtoto Malaika Adam Issara mara baada ya kuwasili Jijini Pretoria kwa ajili ya ziara ya Kiserikali nchini Afrika Kusini tarehe 15 Machi, 2023.
Rais Samia akipokea shada la maua, Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipewa heshima baada ya kuwasili nchini Afrika ya kusini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiimba pamoja na baadhi ya Watanzania wanaoishi Pretoria nchini Afrika Kusini (Diaspora) mara baada ya kuwasili nchini humo tarehe 15 Machi, 2023.

Maboresho Bima ya Afya: NHIF yatoa ufafanuzi
Singida Big Stars yaikana Young Africans