Tatizo la ngapi wa maji katika huji la Dar es Salaam limechangiwa na hali ya ukame wa muda mrefu kwa kiasi kikubwa, na kusema suala hili ni janga lisilozuilika na si kuilaumu CCM.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala na kuwataka wakazi wa jiji hilo kuendelea kuwa wavumilivu wakati mamlaka zikitafutasuluhu.
Makala ambaye alikuwa akionngea mbele ya Rais Samia katika ufunguzi wa mjadala wa kitaifa wa nishati safi ya kupikia amesema suluhu ya kudumu inaandaliwa baada ya hivi karibuni kusainiwa kwa mradi mkubwa wa maji.
Amesema, “Mheshimiwa Rais ni kweli tuna changamoto ya maji na ulituagiza kwa kutupa wiki mbili kutatua jambo hilo nakuhakikishia tunapambana na tutafanikisha kuondosha kero hii.
Aidha, Makala ameongeza kuwa ukosefu huo wa maji unatoka na maeneo mengi kuwa makame hivyo kuathiri vyanzo vingi vya maji na kusema mamlaka ya hali ya hewa ilitangaza jambo hilo na hivyo CCM isilaumiwe.