Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa pendekezo la kuundwa kwa  kikosi kazi cha kitaifa kitakachoratibu dira na mwenendo wa kitaifa wa kuchakata sera na kuleta matokeo chanya ya kuwa na asilimia 90 ya watanzania watakaokuwa wakitumia Nishati safi ya kupikia katika kipindi cha miaka 10 ijayo.

Rais Samia ameyasema hayo hii leo Novemba 1, 2022 wakati akizindua mjadala wa kitaifa wa Nishati safi ya kupikia unaofanyika kwa siku mbili Novemba 1-2, 2022 ukilenga kujadili namna ya kumtua mama mzigo wa kuni kichwani na kuhamasisha matumizi ya gesi.

Amesema sehemu kubwa ya jamii nchini hasa maeneo ya Vijijini imekuwa ikikata miti kwa ajili ya kuni kutokana na bei ya mkaa kuwa chini na hivyo kuhimiza upandaji wa miti ya matunda ambayo wengi wao hawatoweza kuikata bila sababu ya msingi na kwafanya watumie nishati ya gesi kupikia.

“Nimemsikia hapa Dada yangu Tubaijuka akisema katika kitabu chake alichokiandika kwamba alisisitiza umuhimu wa kupanda miti ya mkaa, sasa mimi nataka kubadili fikra tupande miti ya matunda maana hiyo huwezi kuikata bila sababu maalum, tuwahimize watu watumie nishati safi ya kupikia,” amesisitiza Rais Samia.

Aidha, ameitaka Wizara ya Nishati kuhakikisha inahamasisha matumizi hayo ya nishati safi ya kupikia kwa taasisi mbalimbali nchini ikiwemo Magereza, Mashule na Maofisini ili kupunguza matumizi ya mkaa ambao unapatikana kutokana na miti ambayo husaidia uhifadhi wa mazingira.

Kuhusu shida ya maji, Rais Samia amesema tayari mkataba wa ufanyaji kazi umesainiwa ili kukamilisha ujenzi wa Bwawa la kidunda litakalosaidia kupunguza kero ya maji jijini Dar es Salaam na maeneo jirani na kusaidia kusongesha mbele gurudumu la maendeleo.

Ukame chanzo tatizo la maji Dar es Salaam: Makala
Nelson Okwa yamkuta mengine Simba SC