Visa vya dhuluma za kijinsia, vimezidi kuongezeka kutokana na matatizo ya afya ya kiakili kwa wafugaji waliopoteza mifugo yao kutokana na makali ya ukame wa muda mrefu unaoshuhudiwa Marsabit nchini Kenya.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Shirika la kutetea haki za Binadamu la MWADO, Nurria Golloh na kuongeza kuwa, hatua hiyo imesababisha kuanzishwa kwa harakati za kuwafikia wafugaji kwa ushauri nasaha kama sehemu ya kupunguza visa hivyo ambavyo zimeendelea kuongezeka Marsabit.

Amesema, “Tangu wakati wa janga la COVID 19 na ikafuatiwa na ukame wa muda mrefu,kesi za dhulma zimeongezeka kabisa.Familia nyingi zimesambaratika kwa sababu watu wamepoteza mifugo yao.”

Ukame katika eneo la pembe ya Afrika. Picha ya Simon Maina/ AFP.

Kwa upande wake, Afisa Mkuu Mtendaji wa Shirika la Kijamii la CIFA, Salad Liban amemesema visa vya dhuluma za kijinsia zimekosa kuripotiwa katika idara ya polisi akifafanua kuwa,wafugaji wengi hawapendi maswala ya kuelekea mahakamani kutafuta haki.

Amefafanua kuwa, “Kuna ongezeko la dhulma za kijinsia kwa sababu watu walikuwa na mifugo na waliwapoteza.mama akiitisha pesa,mzozo unaibuka.”

Marsabit, ni miongoni mwa majimbo ishirini na tatu yaliyoorodheshwa kuwa katika hali mbaya ya ukame wakati huu.

Stephen Sey aacha deni Geita Gold FC
Marhaba wazinduliwa Algeria