Mwenyekiti Wa Sekta Binafsi Tanzania – TPSF, Angelina Ngalula amesema Watanzania zaidi ya asilimia 90 wapo kwenye kundi la sekta binafsi wakilenga kutengeneza faida, huku mdau namba moja akiwa ni serikali kwenye biashara wanazozifanya.

Angelina ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akichangia mada juu ya sakata la DP World juu ya uendeshaji wa Bandari nchini, na kuongeza kuwa Serikali inakuwa mdau namba moja kwani asilimia 30 ya Biashara zote ni lazima zifike serikalini kwa njia ya kodi.

Mwenyekiti Wa Sekta Binafsi Tanzania – TPSF, Angelina Ngalula.

Amesema, “China ilikaribisha wawekezaji kutoka Marekani [na sehem nyingine duniani]. Wakaenda China wakafungua viwanda, wakatengeneza ajira. Taratibu wachina wakajifunza teklojia na vitu vingine. Baada ya muda wachina wame ‘take-over’ na nchi imekwenda kwa kasi.”

Hata hivyo ameongeza kuwa, nchini Tanzania hata mtoto wa maskini na asiyekuwa na jina, anaweza akamiliki mali akitolea mfano maisha yake kwa kuwa kizazi cha kwanza kwenye familia yao kufanya biashara.

“Lakini leo nimeweza kufanya biashara na kumiliki makampuni makubwa hapa Tanzania na nje ya Tanzania. Hii Ndio Tanzania tunayoitaka.” alisema Mwenyekiti huyo Wa Sekta Binafsi Tanzania – TPSF, Angelina Ngalula.

Mohamed Bares ajipigia debe Ligi Kuu
Kwa jambo hili tutarajie maandamano - Balozi Njenga