Ukraine inaadhimisha tarehe mbili muhimu hii leo Agosti 24, 2022 za kumbukumbu ya miaka 31 ya uhuru wa nchi hiyo kutoka kwa Umoja wa Kisovieti na miezi sita ya vita vilivyoanzishwa na Urusi.
Hali ya hofu inayotanda, wakati wa maadhimisho ya uhuru inaendela huku Maafisa wa Ukrainian na Marekani wakionya kwamba, huenda Urusi ikatumia siku hiyo kuonyesha nguvu, huku Rais Volodymyr Zelensky akiapa kwamba watachukua hatua za haraka na kujibu mapigo ikiwa Moscow itaipiga Kyiv.
Madaktari wathibitisha rasmi uwepo wa Ebola
Waukraine, wana wasiwasi kuwa huenda mashambulizi ya makombora yakaja kujibu mfululizo wa mashambulizi ya Ukraine, dhidi ya malengo ya kijeshi ya Urusi huko Crimea, na uwepo wa uvumi kuwa Ukraine ilimuua mchambuzi wa hawkish, Daria Dugina, na kuongeza mvutano wa kulipa kisasi.
Hata hivyo, utoaji wa maoni umeendelea kote Ukraini, usalama unaimarishwa, Maafisa wa usalama wakiwa mitaani, sherehe za mikusanyiko zikipigwa marufuku na watu kuhimizwa kuzingatia mambo maalumu kama ving’ora vya uvamizi wa anga, jambo ambalo linapuuzwa na wakaazi wengi wa miji iliyo mbali na Kyiv.
Mapema hapo jana, Agosti 23, 2022 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilifanya mkutano wa dharura kujadili juu ya hali ya mapigano yanayoendelea, karibu na kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia kusini mwa Ukraine ili kuepusha maafa yanayoweza kujitokeza.