Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa Tanzania haifanyi vizuri kwenye suala la ukusanyaji wa mapato ukilinganisha na baadhi ya nchi barani Afrika kulingana na pato lake la taifa.

Amesema kuwa Tanzania ndiyo nchi yenye wastani mdogo wa kukusanya kodi, ambapo inakusanya asilimia 12 ya kodi huku ikiwa na jumla ya walipa kodi milioni 2 kati ya watanzania milioni 54. Taifa la Afrika Kusini ambalo lina watu milioni 56, wastani wake wa ukusanyaji wa kodi ukiwa ni asilimia 26.

“Mfano kodi ya majengo ni kubwa sana, majengo yaliyosajiliwa mpaka sasa ni milioni 1.6 napenda kurudia kodi ya majengo iwe shilingi elfu 10 kwa nyumba ya kawaida, na shilingi 20 kwa nyumba za juu na shilingi elfu 50 kwa nyumba za mjini, zitozwe kulingana na hati ya kiwanja, na si idadi ya nyumba kwenye kiwanja,”amesema JPM

Hata hivyo, Rais Magufuli amekutana na Wakuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Mawaziri pamoja na Wakuu wa Mikoa mbalimbali lengo likiwa ni kujadili namna ya kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

 

 

LIVE: Waziri Mkuu katika Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binaadamu Kitaifa
Serikali yalipa zaidi ya shil. bilioni 83 kwa wakulima wa Korosho