Naibu Waziri Wizara ya Uvuvi na Mifugo amezitaka halmashauri kutumia fursa za ufugaji kuwa sehemu ya kuongeza kipato.
Ameyasema hayo katika ziara yake Uvinza mkoani Kigoma ambapo amezitaka halmashauri zote nchini kuthamini ufugaji na kuanzisha lanchi ambazo zitakuwa kichocheo kikubwa cha ukusanyaji mapato.
Amesema kuwa kama fursa hiyo itatumika vizuri basi halmashauri nyingi zitapiga hatua kubwa katika suala la maendeleo.
Aidha, ameipongeza halmashauri ya Uvinza kwa kuwa wabunifu ili kuweza kuongeza ukusanyaji wa mapato kwa kuanzisha lanchi ndogo ndogo.
“Nawapongeza sana halmashauri ya Wilaya ya Uvinza kwa kuwa wabunifu, mimi na Waziri wangu Luhaga Mpina na watendaji wote wa wizara tumejipanga kumaliza migogoro ya wafugaji na wakulima,”amesema Ulega
Hata hivyo, ameongeza kuwa Wizara ya Uvuvi na Mifugo imejipanga kuweza kumaliza matatizo mbalimbali ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara kati ya Wakulima na Wafugaji.
-
Jafo aagiza wakuu wa mikoa kukabiliana na ombaomba
-
Makonda kutengeneza ajira vikundi vya kukimbia
-
Mkapa: Elimu yetu ina ‘mushkeli’