Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 16, 2022 akiwa katika muendelezo wa ziara ya kikazi katika mkoa wa Singida, amekagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji wa Ulemo-Misigiri unaotekelezwa na mkandarasi DDCA – RUWASA.
Mradi huo ambao ulianza kutekelezwa Februari 8, 2021 unatarajiwa kukamilika Agosti 23, 2022 na kwa sasa umefikia asilimia 94 ya utekelezaji.
Mradi huu ambao unatekelezwa kwa fedha za Serikali kupitia mfuko wa maji wa Taifa utagharimu shilingi milioni 569.3 ambapo awamu ya kwanza ilihusisha uchimbaji wa visima vitatu vyenye uwezo wa kuzalisha lita 41,158 kwa saa.
Shughuli zilizotekelezwa mpaka sasa ni Ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 400,000 umefikia asilimia 99, Ujenzi wa tanki la kabla(Sump tank) lenye ujazo wa lita 45,000 umefikia asilimia 96, Ujenzi wa vituo viwili ya kusukuma mitambo umefikia asilimia 100
Shughuli nyingine ni ununuzi na ufungaji wa miundombinu ya kuzalisha maji(lita 30,000 kwa saa na lita 17, 000 kwa saa) umefikia asilimia 100, Ununuzi na ulazaji wa mabomba ya kusafirisha maji yenye urefu wa mita 2,850 umefikia asilimia 99, Ununuzi na ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji yenye urefu wa mita 10,400 umefikia asilimia 100.