Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema katika Jimbo la Singida Kaskazini Vijiji 6 vimesalia kuunganishwa na umeme kati ya vijiji 84 vya jimbo hilo.
Kapinga ameyasema hayo wakati akisalimia wananchi katika Kijiji cha Sagara, wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Singida iliyoanza leo Oktoba 15, 2023.
Amesema Vijiji vyote nchini ambavyo havina umeme vitapata umeme kupitia miradi mbalimbali ya usambazaji umeme vijijini, inayoendelea ukiwemo mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu mzunguko pili.
Serikali kupitia Wizara ya Nishati imeendelea kuhakikisha Vijiji vyote vinavyotakiwa kuwa na Umeme vinapata hitaji hilo muhimu, kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi kwa Taifa na kijamii.