Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto amesema kuwa kitendo alichokifanya Mbunge wa jimbo la Ulanga, Goodluck Mlinga si cha kiungwana kwani yeye hajasomea tasnia hiyo na wala kitendo hicho si sahihi.
Ameyasema hayo baada ya watumiaji mbalimbali wa mitandao ya kijamii kulaani kitendo hicho huku baadhi wakisema ni kucheza na afya za watu, kutokana na mtu asiye na utaalamu wa kitabibu kufanya shughuli hiyo.
Aidha, Ummy amesema kuwa amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya atoe maelekezo ili kuhakikisha kuwa kanuni za kitabibu zinazingatiwa.
“Hii sio sahihi. tayari nimeshamuelekeza Katibu Mkuu Afya kutoa maelekezo mara moja kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kusisitiza uzingatiwaji wa Miongozo ya kitaalamu yafanywe na Wataalamu”.amesema Ummy Mwalimu
-
Serikali yapata mwekezaji mpya mradi wa mabasi ya mwendokasi
-
Serikali kumwaga ajira za Walimu shule za msingi
-
Magufuli aomba kuombewa asiwe na Kiburi