Serikali imesema kuwa Juni 30, 2018 inatarajia kutoa ajira 10,140 za walimu wa shule za msingi nchini ili kuweza kukabiliana na tatizo hilo.

Hayo yamesemwa leo Mei 2, 2018 Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Tamisemi, Joseph Kakunda wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Ludewa (CCM), Deogratius Ngalawa.

Katika swali lake, Ngalawa alitaka kupata majibu ya Serikali kuhusu upungufu wa walimu 500 wa shule za msingi na jinsi litakavyo shughulikiwa.

Hata hivyo, Kakunda amesema kuwa serikali itaendelea kushirikiana na Baraza la Mitihani la Taifa kwa kupitia vyeti vya vya walimu na wanategea kufikia juni 30 kuweza kuwa ajili.

 

 

 

 

Serikali yapata mwekezaji mpya mradi wa mabasi ya mwendokasi
Magufuli aomba kuombewa asiwe na Kiburi