Baada ya Asma Juma, mzazi aliyedai kuibiwa pacha wake mmoja katika hospitali ya Temeke na kuishitaki hospitali hiyo, Ummy mwalimu aliagiza uchunguzi ufanyike na akibidhiwe ripoti kuhusu tafiti hiyo.
Leo Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa majibu ya ripoti iliyoleta utata kati ya mzazi huyo na madaktari wa hospitali ya Temeke, Ummy Mwalimu amesema ripoti imebaini kuwa mama huyo alikuwa na mimba ya mtoto mmoja.
-
Naibu Waziri afanya ziara ya kushtukiza mradi wa umeme Kinyerezi II, atoa agizo
-
CCM yamng’ang’ania Lowassa, mwenyewe akomaa na yake
Ambapo ufafanuzi zaidi umetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya Uchunguzi Profesa Charles Majinge, na kusema kuwa kulikuwa na makosa yaliyofanyika kipindi wanamfanyia mama huyo vipimo vya utrasound ambapo vipimo hivyo vilivyobaini kuwa mama huyo ana watoto mapacha ilihali vilitakiwa kubainisha kuwa ana mtoto mmoja.
Kabla ya kutoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari, Waziri Mwalimu na Profesa Majinge walikutana na familia ya Asma na kuwapatia matokeo ya ripoti, matokeo ambayo hata hivyo yamemfanya mama huyo kuangua kilio.