Jeshi la Polisi linawaska watuhumiwa 16 wa mauaji ambayo yamekuwa yakiendelea kufanyika katika maeneo ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji Mkoani Pwani kwa muda mrefu sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni  amesema kuwa watuhumiwa hao wanafahamika na tayari Jeshi la Polisi lina majina na picha za watuhumiwa wote ambao wanasakwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro, amesema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha linatokomeza vitendo hivyo vya uhalifu, pia amewapongeza wanachi kwa kuanza sasa kuonyesha ushirikiano kwa kutoa taarifa ambazo hadi sasa zinasaidia jeshi hilo.

Masauni anena mazito kuhusu mauaji ya Kibiti, Rufiji na Mkuranga
Ummy Mwalimu aripoti kuhusu mzazi aliyeibiwa pacha Temeke