Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameagiza kuanzishwa duka la dawa ndani ya miezi 3 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.

Ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Iringa ambapo ametembelea Kituo cha  Damu Salama cha Mkoa pamoja na Hospitali ya Wilaya ya Mafinga

“Naagiza Uongozi wa  Hospitali zote za Mikoa na Wilaya kuanzisha Wodi za Watoto Wachanga na Watoto Njiti mara moja” amesema Ummy.

Aidha, Mbali na hayo Ummy  ameagiza kujengwa kwa  Kitengo cha Wagonjwa wa dharura (Emergency Unit) kwa hospitali hizo mara moja ili kuboresha huduma ya afya kwa wakazi wa Iringa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza  amesema kuwa hatua mbalimbali wanazochukua katika kuboresha utoaji wa huduma ikiwemo kuboresha miundombinu ya vituo vya Afya, upatikanaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba, utoaji wa elimu ya uzazi wa mpango pamoja na lishe kwa wananchi na kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).

Hata hivyo, amesema kuwa zipo changamoto kadhaa zinazowakabili mkoa kufikia lengo lao kutoa huduma bora za Afya.

Katika hatua nyingine, Ummy Mwalimu amewapongeza viongozi na watumishi wa mkoa kwa juhudi kubwa wanazofanya katika kuboresha huduma za afya ikiwemo kufanikisha ujenzi wa wodi ya watoto waliozaliwa kabla ya wakati na watoto wachanga.

Balotelli Ageuka Mbongo Baada ya Kuulizwa Kuhusu Liverpool
Joe Hart Amtuliza Andrea Belotti