Mlinda mlango kutoka nchini England, Joe Hart amemshauri mshambuliaji wa klabu ya Torino, Andrea Belotti azipe mgongo taarifa za usajili wake ambazo zinaendelea kuvumishwa na vyombo vya habari duniani kote.

Belotti anahusishwa na taarifa za kuwaniwa na klabu za FC Barcelona, Chelsea na Arsenal.

Hart ambaye anaitumikia Torino kwa mkopo akitokea Man City, amemwambia mshambuliaji huyo kuwa hakuna haja ya kuzipa nafasi taarifa hizo, bali anachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kufikia lengo la kupandisha kiwango chake cha soka.

“Nimemueleza kuhusu maisha yake ya sasa na ya baadae, hakuna haja kufikiria suala la usajili wakati muda wa usajili bado haujafika. Kwa sasa ni wakati mzuri kwake kuendelea kucheza soka kwa manufaa ya kuisaidia Torino, Vyombo vya habari kazi yao ni kutoa taarifa, na wakati mwingine huwa za kweli ama tetesi,” anakaririwa.

“Ninaamini kama Belotti atazipa nafasi taarifa za usajili, kuna hatari ya kushindwa kufikia malengo aliojiwekea na akajikuta akiporoka kiwango,” aliongeza katika mahojiano na kituo cha televisheni cha klabu ya Torino.

Ummy Mwalimu atoa miezi mitatu kuanzishwa duka la dawa
Exclusive: Profesa Jay afunguka kuhusu video ya wimbo wake ‘Kibabe’