Umoja wa Ulaya umeitaka China kubatilisha mara moja sheria zake mpya zilizopelekea kupigwa marufuku kwa wabunge wanna waliochaguliwa, ikisema uamuzi huo ni pigo kubwa kwa utawala wa ndani wa Hong kong.
Katika taarifa, nchi ishirini na saba za Umoja wa Ulaya zimesema hili ni pigo kubwa kwa uhuru wa maoni Hong Kong.
Wabunge wanaopigania demokrasia Hong Kong wamejiuzulu wakipinga marufuku ya wabunge hao iliyotolewa na bunge la mji huo, baada ya serikali ya China kuipa serikali ya mji huo mamlaka mapya kwa ajili ya kuzuia upinzani.
Taarifa hiyo ya Umoja wa Ulaya pia imesema inataka wabunge hao walioachishwa kazi warejeshwe katika nafasi zao mara moja.