Tanzania na Uganda ni miongoni mwa nchi kadhaa barani Afrika zinazochunguzwa kwa kukiuka vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Korea Kaskazini kuhusu ushirikiano wa kibiashara na nchi hiyo.
Ripoti iliyotolewa Septemba 9 siku mbili kabla ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa pamoja kuweka vikwazo vipya vinavyo ishinikiza Korea Kaskazini kufanya mazungumzo juu ya silaha zake za nyuklia.
Aidha, Jopo la watalaamu kutoka Baraza la Umoja wa Mataifa linafanya tathmini juu ya taarifa kutoka kwa vyanzo vya habari vya nchi wanachama wa UN ambavyo havijatajwa majina vikisema kuwa Tanzania iliingia mikataba ya kijeshi na Korea Kaskazini yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 12.5.
Kampuni ya Haegeumgang Trading Corporation inasemekana kuwa inafanya ukarabati na kurekebisha mifumo ya makombora ya kivita na ulinzi wa anga kuifanya iwe ya kisasa zaidi.
-
Korea Kaskazini yatishia kuigeuza Marekani kuwa mavumbi, kuizamisha Japan
-
Ofisi za UN zavamiwa nchini Burundi
Hata hivyo, Jopo hilo limeongeza kuwa linaendelea kufanya uchunguzi wake juu ya Korea Kaskazini kutoa mafunzo ya kijeshi kwa jeshi la Uganda na vikosi vya polisi nchini humo,