Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa la kutetea haki za binadamu zilizopo katika mji mkuu Bujumbura nchini Burundi zimevamiwa na kundi la watu wenye silaha kisha kuvunja vunja milango na kusababisha hasara kubwa.

Tukio hilo limetokea wiki moja mara baada ya shirika hilo kuripoti uwezekano wa kuongezeka kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu nchini Burundi, ikijumuisha mauaji na kukamatwa watu kiholela, utesaji, udhalilishaji wa kijinsia na kupotea kwa baadhi ya watu.

Aidha, Burundi imekuwa katika hali ya taharuki ya kisiasa toka rais wa nchi hiyo, Piere Nkurunzinza kugombea na kushinda katika uchaguzi mkuu uliopita ambapo ataiongoza nchi hiyo kwa muhula wa tatu.

Hata hivyo, hakukuwa yeyote ya kuhusu upotevu wa mali zilizokuwemo katika ofisi hizo au madhara yaliyoripotiwa lakini limesababishiwa hasara kubwa kutokana na uvunjwaji wa ofisi hizo. i

Video: Rick Ross aachia 'Santorini Greece'
Pasipoti za kielektroniki kuzinduliwa rasmi