Katika kizazi cha wafanyakazi mchanganyiko katika ajira, makampuni huamua kuajiri au kupandisha vyeo wafanyakazi wenye ujuzi na uwezo mzuri kikazi kuwa wasimamizi wakuu. Hii hupelekea kuwe na uwezekano wa wewe kuwa na Bosi uliyemzidi umri na huenda usifurahie kwa sababu ya umri wa bosi wako. Tafiti unaonyesha kwamba wafanyakazi katika makampuni yenye mabosi wenye umri mdogo kuliko wao huwa na hisia hasi ikilinganishwa na wale walio na mabosi waliowazidi umri.
Ikiwa wewe na meneja wako mheshimiana, kufanya kazi pamoja haipaswi kuwa tatizo. Hata ikiwa umemzidi umri. Ni muhimu zaidi kuzingatia ukuaji wa kazi yako kuliko kuhangaika juu ya umri mdogo wa bosi wako. Hivi ni vidokezo unavyopaswa kufikiria ili kufurahia kufanya kazi na meneja uliyemzidi umri.
- Waheshimu Inavyostahili
Bosi wako anaweza kuwa na umri mdogo kuliko wewe, lakini si kwamba hana uwezo unaotakiwa. Ni muhimu kusikiliza na kuheshimu maamuzi yake. Hata hivyo, mambo ambayo utafanya ili kuonyesha heshima kwa bosi aliyekuzidi umri hayana tofauti na kwa bosi mwenye umri mdogo kwako. Kubali kuwa yeye ni mtu sahihi kufanya kazi hioyo na daima kuwa muwazi kwa mawazo anayoleta na kukubali kwa mtazamo chanya. Ikiwa unaonyesha heshima kwa bosi wako, ni wazi kabisa kuwa utaipata ya kwake kwa urahisi pia.
2. Uzoefu Wako ni wa Muhimu
Uzoefu wako wa kazi ndani ya kampuni ni moja ya zana muhimu sana ambazo unaweza kutumia katika kuimarisha uzalishaji na ufanisi wa shirika. Unaweza kutumia hii kumsaidia bosi wako mdogo kukuza ujuzi wake katika kuongoza timu na kusaidia kampuni kukua. Bosi wako anaweza kuwa na ujuzi katika eneo fulani kama vile teknolojia lakini hajui mengi kuhusu mawasiliano. Unapaswa kuwa tayari kumfundisha ujuzi uliyopata kwa miaka mingi na atatambua mchango wako kwa kampuni kirahisi zaidi kwa ukuaji bora wa kazi yako baadaye.
- Kubali Kubadilika na Kujifunza Mambo Mapya
- Usifikirie sana Kuhusu Hilo
Maamuzi uliyofanya katika kazi zako ndio yamekusaidia uwe katika nafasi yako ya sasa. Uko katika nafasi hii kwa sababu ya kazi yako na kwamba unapaswa kujivunia. Hutakiwi kufikiri kwamba timu ya uongozi inakuona kuwa duni zaidi kwa sababu walitoa jukumu la ubosi kwa mtu mwingine aliye mdogo kuliko wewe. Kuwa na ujasiri kukubaliana na ukweli kwamba walikuajiri ili kuleta thamani maalum kwa timu. Hakikisha unajaribu kufanya kazi na bosi wako mdogo na kujitoa kwa kila ulicho nacho kufanikisha kazi hiyo.
- Wasiliana Vyema na Mapema
Mawasiliano ya wazi kati ya wewe na bosi wako yatawafanya muweze kuelewana na kujenga mazingira mazuri ya kazi. Tafuta njia yake nzuri ya mawasiliano ili kuunda mazungumzo sahihi, kujenga imani na kuboresha tija ya kampuni.
- Ukuaji wako wa Kazi na Kampuni Ndio Kipaumbele
Mwisho, unapaswa kukumbuka kuwa upo katika nafasi uliyopo kama ulivyokusudia waukianza kazi yako. Daima amini kwamba kazi yako itaendelea kukua bila kujali tofauti ya umri kati yako na bosi wako. Kwa kuongeza, kumbuka kwamba wewe na bosi wako mpo kwenye timu moja na lengo lenu ni moja, kukuza kampuni.