Klabu ya Arsenal imethibitisha kumteua Unai Emery kuwa kocha mpya wa klabu hiyo akichukua nafasi ya Arsene Wenger ambaye amestaafu baada ya kuitumikia Arsenal kwa miaka 22.
Emery mwenye umri wa miaka 46 amejiunga na Arsenal baada ya kuondoka Paris Saint-Germain ambapo aliingoza klabu hiyo kushinda ubingwa wa ligi kuu ya Ufaransa League 1.
Kocha huyo raia wa Hispania amesaini mkataba wa miaka miwili kutumikia Arsenal. Afisa mkuu mtendaji wa klabu ya Arsenal, Ivan Gazidis amesema kocha huyo amekuwa na rekodi bora katika kazi yake na ana mtindo mzuri wa uchezaji mpira utakaoifaa Arsenal.
-
Neymar arejea dimbani, Rivaldo amtabiria ‘Ballon d’Or’
-
Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Iran.
Arsenal wameshindwa kumaliza katika nafasi nne za juu msimu huu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza huku wakitolewa kwenye kombe la Europa League katika hatua ya nusu fainali.
Unai Emery ana rekodi nzuri katika michuano ya Ulaya kwani ameshinda makombe 3 mfululizo ya Europa aliyobeba akiwa na Sevilla mwaka 2014 waliifunga Benfica kwa penati, 2015 wakaifunga Ukrainians Dnipro kisha wakaipiga Liverpool 2016.