Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA ) Hashim Rungwe  amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kutoa tamko la kuruhusu mikutano ya vyama vya siasa. 

Ameyasema hayo leo Julai 7, 2021 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa kitendo Cha kufungiwa kufanya mikutano ya kisiasa kinaminya  haki  yao ya  kikatiba .

Amesema ibara ya tisa (G na H) inasema  kwamba serikali na vyombo vyake vyote vya Umma vinatoa nafasi zilizo  sawa kwa raia wote bila kujali rangi, dini au hali ya mtu na kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu,au upendeleo zinaondolewa nchini.

Hali kadhalika Rungwe akielezea yale aliyoyatekeleza  Rais Samia katika siku mia moja za uongozi  wake amesema ni miongoni mwa kazi za Rais kwa kuwa katiba inamtaka kuyatekeleza.

Hashim Rungwe ni miongoni mwa wanasiasa waliogombea nafasi ya Urais katika uchaguzi uliopita Octoba 2020 kupitia chama cha CHAUMMA hata hivyo kura zake hazikutosha kuwa Rais.

Simba Queens mguu sawa CECAFA
Mzee Samatta: Morrison angetamba sana