Droo ya mchujo wa Kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Soka la wanawake ukanda Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) inatarajiwa kufanyika baadae leo Jumatano (Julai 07).

Tanzania Bara itawakilishwa na mabingwa Simba Queens katika michuano inayotarajiwa kufanyika nchini Kenya kati ya Julai 17 hadi Agosti 1

Simba Queens, Lady Doves FC (Uganda) na Benki ya Biashara ya Ethiopia FC ndio timu zinazopewa nafasi kubwa ya kubeba ubingwa na kukata tiketi moja ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika

Timu nyingine ambazo zitashiriki ni pamoja na; PVP FC (Burundi), FAD Club (Djibouti), Scandinavia WFC (Rwanda), Yei Join Stars (Sudan Kusini) na New Generations FC (Zanzibar)

Timu sita za juu (Moja kutoka kila Kanda ya CAF) na mwenyeji wa mashindano ya mwisho (Misri) pamoja na timu moja ya ziada kutoka Kanda iliyoshikilia taji la Kombe la Mataifa ya Afrika la Wanawake la mwaka uliopita zitafuzu kwenye mashindano ya mwisho ya Ligi ya Mabingwa Afrika Wanawake.

Ikumbukwe kuwa Simba Queens ndio Mabingwa wa Tanzania Bara kwa misimu miwili mfululizo.

Serikali yaendeleza ubunifu kwa vijana
Upinzani wamwangukia Rais Samia