Mabingwa wa Ulaya Ureno wamefuzu kucheza kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Uswizi katika mechi iliyopigwa hapo jana mjini Lisbon.

Hii ni mara ya 9 mfululizo kwa Ureno kushiriki kombe la dunia huku safari hii wakiwa wamefunga jumla ya mabao 32 na kumaliza kileleni mwa kundi B.

Timu ya taifa ya Ufaransa nayo imewapiga Belarus bao 2 kwa 1 na kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia huku wakiweka rekodi ya kutopoteza mchezo hata mmoja katika uwanja wao wa nyumbani wakati wa mechi za kufuzu.

Kwingineko Marekani hawatashiriki michuano ya Kombe la Dunia mwaka ujao nchini Urusi baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 na Trinidad & Tobago katika mechi ya kufuzu kwa michuano hiyo iliyopigwa hapo jana.

Mara ya mwisho kwa Marekani kukosa kushiriki fainali za Kombe la Dunia ilikuwa mwaka 1986.

Arjen Robben astaafu kwa kufunga mawili
Trinidad na Tobago yaizima Marekani, ndoto za 2018 zayeyuka