Iran ilifuzu fainali hizi ikitokea ukanda wa bara la Asia, baada ya kuongoza kundi A (kundi la Kwanza) lililokuwa na timu za Korea Kusini, China, Syria, Uzbekistan na Qatar.

Ilifanikiwa kumaliza ikiwa kinara wa kundi hilo kwa kufikisha alama 22, ikifuatiwa na Korea Kunisi waliopata alama 15, Syria alama 13, Uzbekistan alama 13, China alama 12 na Qatar ilimaliza nafasi ya mwisho kwa kuwa na alama 7.

Jina la utani la timu ya taifa ya Iran: Team Melli

Mfumo: Kikosi cha Iran hutumia mfumo wa 4-2-3-1.

Image result for Sardar AzmounMchezaji Nyota: Sardar Azmoun (Rubin Kazan).

Image result for Saman Ghoddos -iranMchezaji hatari: Saman Ghoddos (Ostersund).

Image result for Masoud Soleimani Shojaei -iranNahodha: Masoud Soleimani Shojaei (AEK Athens FC)

Image result for Carlos Manuel Brito Leal QueirozKocha: Carlos Manuel Brito Leal Queiroz (65), raia wa Ureno.

Ushiriki: Iran wameshiriki fainali za kombe la dunia mara nne (4). Mwaka 1978, 1998, 2006 na 2014.

Mafanikio: Hatua ya Makundi.

Kuelekea 2018:

Hii inakuwa mara ya pili mfululizo kwa taifa la Iran kushiriki fainali za kombe la dunia, baada ya kufanya hivyo mwaka 2014 nchini Brazil.

Iran ilikuwa timu ya taifa ya kwanza kufuzu fainali za mwaka huu ukanda wa Asia, huku wakicheza michezo 12 ya kuwania kufuzu bila kufungwa. Hali inayodhihirisha wana safu nzuri ya ulinzi na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.

Kabla ya kuelekea urusi, kikosi cha Iran kinachonolewa na Queiroz kitajipima ubavu dhidi ya Urusi, Panama na Venezuela, ili kujiweka vyema katika mfumo wao wa 4-2-3-1.

Japo katika mchezo wa soka lolote linaweza kutokea, lakini Iran hawapewi nafasi kubwa ya kufanya vyema katika fainali za mwaka huu, kutokana na kuwa na historia isiyopendeza.

Hata hivyo, Iran imeonesha kupanda baada ya kutajwa kuwa timu yenye kiwango cha juu zaidi katika bara la Asia tangu Disemba 2014. Kwa sasa imeshika nafasi ya 32 duniani katika viwango vya FIFA.

Iran itaanza kampeni za kuusaka ubingwa mwaka huu kwa kucheza dhidi ya Morocco, Uwanja wa Krestovsky, mjini Saint Petersburg Juni 15, kisha watapambana na Hispania Juni 20, Uwanja wa Kazan, mjini Kazan, na mchezo wao wa mwisho hatua ya makundi watapapatuana na Ureno Juni 25, Uwanja Mordovia, , mjini Saransk.

Tunakamilisha uchambuzi mfupi katika timu B. Mfululizo wa makala hizi utaendelea kesho kwa kumulika timu nyingine hadi tutakaposikia sauti ya Kipyenga cha kuashiria kuanza rasmi kwa mechi ya kwanza ufunguzi wa Kombe la Dunia.

Endelea kuwa na Dar24, tembelea YouTube channel yetu ya Dar24 Media kupata mengi zaidi.

 

 

Neymar arejea dimbani, Rivaldo amtabiria 'Ballon d'Or'
Wafungaji hatarini kupata saratani ya utumbo, Daktari atoa ushauri