Rais wa Urusi, Vladmir Putin, amesema nchi yake itaweka mazingira bora zaidi ya uwekezaji miradi mikubwa ya vinu vya kuchakata bidhaa mbalimbali zitokanazona mafuta ya petroli.
Amesema ili kufanikiwa katika miradi hiyo, kuna mambo mawili ya kuzingatia na jambo la kwanza, ni wakati gani mwafaka wa kuanza kazi hiyo na jambo la pili, nigharama za kazi hiyo ambazo serikali lazima ikabiliane nazo.
Kiongozi huyo aliyasema hayo wakati alipokuwa akifungua mkutano mjini Moscow kuhusu mikakati ya maendeleo katika sekta ya petroli na bidhaa zitokanazo namafuta hayo yanayotumika zaidi duniani.
“Mamlaka za Urusi zitaendelea kujenga mazingira rafiki kwa ajili ya kuvutia wawekezaji kwa ajili ya kuendeleza taifa letu kiuchumi,” amesema Putin.
Amesema kupitia vinu hivyo vitakavyojengwa na wakandarasi wa Urusi, taifa hilo litaongeza uwezo wake wa kusafisha mafuta ya petroli ambapo bidhaa kadhaazitapatikana kwa maendeleo ya Urusi na watu wake.
Kwa mujibu wa Putin, miongozo na taratibu za kiujenzi ambazo zimepitwa na wakati zitaachwa na kutumia mfumo na teknolojia za kisasa zaidi ili kurahisishauzalishaji utakaokuwa na tija na wa kudumu kwa miaka kadhaa ijayo.