Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema inasitisha mashambulizi yake saa 10 asubuhi kwa saa za huko siku ya Jumamosi ili wakazi waweze kuondoka katika bandari ya Azov ya Mariupol iliyozingirwa na vikosi vya Urusi, karibu kilomita 110 kutoka Donetsk.
Urusi inatambua jiji hilo kama sehemu ya Jamhuri ya Watu wa Donetsk (DPR). Hatahivyo, imekuwa ikidhibitiwa na Ukraine tangu 2014.
Moscow imesema kuwa njia salama zilikubaliwa na Ukraine ambapo Raia wa Urusi na Ukraine walikutana kwa duru ya pili ya mazungumzo ya amani huko Belarus siku ya Alhamisi.
Maafisa wa Mariupol wamesema raia hao wana hadi saa kumi jioni kwa saa za ndani kuondoka kwa gari au basi kupitia njia tatu za uokoaji Uhamisho huo utafanyika “katika hatua kadhaa za siku kadhaa,” maafisa walitangaza.
Meya wa Mariupol Vadim Boychenko amesema usitishaji huo wa mapigano utaruhusu kazi kuanza kurejesha usambazaji wa umeme na maji, pamoja na huduma ya simu ya mkononi.
Ameongeza kuwa maafisa wa eneo hilo pia watatoa huduma ya kupeleka chakula na vifaa vya huduma ya kwanza.