Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Urusi, Sergei Lavrov amemwambia waziri wa Ulinzi wa Marekani, Rex Tillerson kuwa kuiwekea vikwazo vingi Korea Kaskazini hakutasaidia chochote kutatua mgogoro uliopo kuhusu mpango wake wa nyuklia.

Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje nchini Urusi imesema kuwa viongozi hao wamezungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio yanayofanywa na Korea Kaskazini.

Lavrov amesema kuwa diplomasia ndio njia pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana.

Hata hivyo, Waziri wa ulinzi wa Marekani amesema kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini ili iweze kuachana na mpango wake wa majaribio ya silaha za nyuklia huku Rais Trump akisema mazungumzo sio suluhisho.

 

Haji Manara afichua siri ya benchi la ufundi
Arsene Wenger: Bila Kun Aguero Sanchez hang'oki