Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani kitendo cha Korea Kaskazini cha kurusha kombora kupitia anga ya Japan, huku nchi hiyo ikithibitisha kutekeleza urushaji wa kombora hilo.

Aidha, katika kuhakikisha kuwa kuna hali ya amani ukanda huo, Baraza la Usalama limeitaka Korea Kaskazini kusitisha mara moja majaribio yake na mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia ambazo zimekuwa zikipingwa vikali na Marekani.

Mataifa Wanachama 15 ya Baraza hilo la Usalama wameadhimia kuichukulia hatua kali na haraka Korea Kaskazini dhidi ya mpango wake huo ambao umekuwa ni tishio kwa nchi jirani na baadhi ya mataifa ili kuweza kupunguza hali ya wasiwasi.

Hata hivyo, Majeshi ya Korea Kusini na Marekani bado yanaendelea kufanya mazoezi ya pamoja karibu na mpaka wa Korea Kaskazini, jambo ambalo Pyongyang inasema ni maandalizi ya uvamizi.

 

Wapinzani kushtakiwa kwa makosa la uhaini
Magazeti ya Tanzania leo Agosti 30, 2017