Serikali nhini Urusi, imekataa kikomo cha bei ya mafuta iliyowekwa na mataifa ya Magharibi yanayoiunga mkono Ukraine, huku ikitishia kuacha kusambaza mafuta katika mataifa yote yaliyodhinisha hatua hiyo.
Kwa mujibu wa msemaji wa ikulu ya Urusi, Dmitry Peskov amesema wataitathmini hali hiyo kabla ya kutangaza maamuzi yake juu ya hatua itakazochukua, na kusisitiza kuwa haitakubali hatua iliyoidhinishwa.
Desemba 2, 2022, jumla ya Mataifa 27 ya Umoja wa Ulaya, ikiwemo Australia, Japan, Uingereza na Marekani, yalikubaliana kuweka ukomo wa bei ya mafuta ya Urusi, ili isipindukie dola 60 kwa pipa moja.
Hata hivo, ofisi ya Rais wa Ukraine, Volodymyrr Zelensky hapo jana (Desemba 3, 2022), ilitoa wito wa kuongezwa zaidi ukomo wa bei ya mafuta ya Urusi, akisema bei iliyopitishwa na washirika wake haifai.