Uongozi wa KMC FC umepania kuboresha kikosi chao kuelekea msimu ujao baada ya kutenga kiasi cha Sh Bilioni moja kusajili wachezaji wapya.

KMC FC imetenga kiasi hicho cha fedha baada kutofurahishwa na mwenendo wa timu hiyo katika misimu miwili iliyopita ambapo msimu wa 2021-22 walimaliza msimu nafasi ya 10 kabla ya uliopita kulazimika kucheza mechi za mtoano kusalia Ligi Kuu Bara.

Afisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wanahitaji kuwa wa tofauti kuelekea msimu ujao na zaidi wanahitaji wachezaji mahiri kwa ajili ya kuongeza makali zaidi kwa timu hiyo.

“Msimu ujao hatutaki kuona kama yaliyotokea msimu uliomalizika ndiyo maana tumeamua kuongeza bajeti yetu ya usajili na kufikia Sh bilioni moja, na hatutasubiri mchezaji aachwe kwingine na sisi tumsajili bali tukimuona mchezaji anatufaa, tutakwenda kuvunja mkataba kwa waajiri wake na kumsajili,” amesema Christina.

Aidha, imeelezwa kuwa kufikia bajeti hiyo, KMC FC imeongeza kiasi cha Sh milioni 300 kutoka milioni 700 ya bajeti yao ya usajili ya msimu uliopita, ikihitaji kuongeza ushindani katika ligi hiyo inayotajwa kuwa ni ya tano kwa ubora barani Afrika kwa sasa.

Kocha Gamondi kuamua usajili wa Mkude
TFF yafunguwa dirisha la usajili 2023/24