Klabu ya Manchester United inaangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa England na klabu ya AS Roma ya Italia Tammy Abraham.

Abdaham anakuwa chaguo la pili katika usajili wa Man Utd, endapo klabu hiyo itashindwa kukamilsha mpango wa kumsajili Mshambuliaji wa Spurs Harry Kane.

Meneja wa Man Utd Erik ten Hag anataka kumpata mshambuliaji namba tisa wakati timu hiyo ikihusishwa na kumtaka nahodha wa timu ya taifa ya England, Kane.

Mshambuliaji kutoka nchini Nigeria na klabu ya SSC Napoll, Victor Osimhen anatajwa kuwa katika orodha ya Meneja huyo kutoka nchini Uholanzi.

Hata hivyo endapo Sheikh Jassim akifanikiwa kuinunua Klabu ya Man Utd huenda akamsajili nyota wa PSG Neymar ambaye anapigiwa chapuo la kuondoka jijini Paris mwishoni mwa msimu huu.

Nyota wa zamani wa Chelsea, Abraham, 25, anatajwa kuwa katika orodha ya Mashetani Wekundu, ambao walituma watu kumtazama akiwa katika majukumu yake nchini Italia.

Songo awania rekodi ya tatu Championship
Alvarez Julian: Tumefika tulipopataka