Azam FC imekamilisha usajili wa washambuliaji Alassane Diao, Gibril Sillah na Feisal Salum jambo ambalo ni kama vile wadau wengi wanaona wanajaza wachezaji wengi kwenye eneo hilo.

Hadi sasa kwenye eneo la ushambuliaji, Azam FC ina Abdul Suleiman ‘Sopu’, Idris Mbombo na Prince Dube, ambao wote ni wachezaji wa umaliziaji huku wakiwa na uwiano mzuri wa kuweka mipira wavuni.

Uongozi wa Azam FC kupitia kwa msemaji wa timu hiyo, Hasheem Ibwe umeweka wazi kwamba kuongeza eneo lao la ushambuliaji ni kuzidi kukiimarisha kikosi chao.

“Tunatafuta uimara zaidi, tulikuwa kama nusu kwa nusu kwa hiyo tunaimarisha kikosi kwa ajili ya msimu ujao na ndiyo maana unaona wameingia,” alisema Ibwe

Wakati Ibwe akisema hayo, Azam FC imemsajili Cheikh Sidibe, ambaye ni beki wa kushoto akirithi mikoba ya Bruce Kangwa ambaye hajaongezewa mkataba.

Licha ya Azam FC kuwa na washambuliaji wengi, eneo la ulinzi wa kati lina wachezaji watatu pekee, Malick waa msimu wa Ndouye, Daniel Amoah na Abdallah Kheri ‘Sebo’.

Azam FC inamtumia Lusajo Mwaikenda kama beki wa kulia, licha ya kwamba uhalisia wake ni beki wa kati, lakini hilo linatokana na beki wa kulia, Nathan Chilambo kutokuwa na uwiano wa uhakika kwenye kikosi chake.

Azam FC humtumia Edward Manyama kama beki wa kati, licha ya kwamba ni beki wa kushoto na hilo lilitokana baada ya kukosa uhakika wa namba mbele ya Bruce Kangwa.

Kikosi hicho chenye maskani yake Chamazi msimu uliopita kilifunga mabao 55 na kuruhusu 29 katika Ligi Kuu na kuwa timu ya nne ambayo imeruhusu mabao machache.

Simba SC ndiyo timu iliyoruhusu mabao machache zaidi (17), wakati Young Africans ikiwa ya pili 17 na ya tatu ni Singida Big Stars iliyofungwa mara 26.

Lautaro Martinez kukabidhiwa mikoba Real Madrid
Neymar alimwa faini ya mazingira Brazil