Halmashauri za Mkoa wa Kagera, zimetakuwa kuwatumia watendaji wa vijijini pamoja na maafisa ugani ili kuongeza nguvu Siku za minada ili kudhibiti ukwepaji wa ushuru na kuwabaini wafanyabiashara wa mifugo ili wakatiwe na kulipia leseni zao.
Hayo yameelezwa na Naibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa- TAKUKURU mkoa wa Kagera Ezekia Sinkala wakati akitoa taarifa kwa umma juu ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi, 2023.
Ajali: Kiboko agonga mtumbwi, 20 wahofiwa kufa maji
Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kagera, Ezekia Sinkala.
Amesema, “tuliweza kufanya uchambuzi wa mfumo wa mianya ya upotevu wa mapato katika minada ya mifugo, tuliweza kubaini kwamba kuna usimamizi usio imara kwa wafanyabiashara wa mifugo ambapo kunakuwa na upotevu wa ushuru.”
Wafanyabiashara hawabainishwi sawasawa na hivyo anapoenda kuuza mifugo yake anaweza kulipia ushuru mifugo michache kuliko aliyouza lakini pia tumebaini hawana leseni tumeshauri Halmashauri zinazohusika wafuatilie ili kuwabaini ambao hawana leseni,” amesema.
Waandishi wa habari wa Mkoa wa Kagera wakimsikiliza Naibu Mkuu wa TAKUKURU, Ezekia Sinkala.
Aidha ameongeza kuwa, “kuna mianya ya upotevu wa mapato katika masoko ya biashara ambapo mianya iliyobainika ni halmashauri inakosa mapato kwa kutotoza ushuru katika baadhi ya masoko kwa mfano soko la ndizi Murongo wilaya ya Kyerwa na soko la Kabindi katika wilaya ya Biharamulo.”
Katika taarifa hiyo, jumla ya miradi 52 ya maendeleo yenye thamani ya Shilingi 9.2 bilioni inayotekelezwa mkoani Kagera imefatiliwa na TAKUKURU ambapo miradi sita yenye thamani ya 1.5 bilioni ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya maji, hospitali, vituo vya afya na ujenzi wa madarasa shule za sekondari.
Ujenzi huo umebainika kuwa na mapungufu huku malalamiko 43 yakihusu rushwa na kufunguliwa majalada ya uchunguzi na uchunguzi wa majalada 38 umekamilika na hatua mbalimbali za kisheria zinatarajia kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa pia majalada 5 uchunguzi wake bado unaendelea.