Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema mambo muhimu katika nchi yoyote Duniani ni pamoja na uwepo na kuitunza amani, kudumisha umoja na na Wananchi kuwa na mshikamano.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema katika dua ya kuiombea Nchi na Viongozi, iliyoandaliwa na Wazee wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wakiwemo Maimamu na Waalimu wa Madrasa za Mkoa huo liyofanyika Msikiti wa Ijitimai Kidoti, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema, anawashukuru waumini waliojitokeza katika dua hiyo na kufarajika kuendelea kuwaombea Viongozi dua, ili watimize ahadi zao kwa Wananchi na kusaidia upataji wa maendeleo tarajiwa.
Aidha, Dkt. Mwinyi pia amewahimiza waumini hao kuendelea kumuomba Mungu juu ya mmong’onyoko wa maadili katika jamii, na kuwataka wazazi na walezi kuwafundisha elimu ya dini watoto na vijana, ili wawe na hofu ya Mungu na kuwa na maadili mema.