Suala la Utawala Bora katika nchi limetajwa kuwa si sera madhubuti na kanuni nzuri pekee, bali ni kunahitajika kuwepo ufanisi kwenye utoaji na ufikishaji wa huduma kwa wananchi pamoja na utawala maridhawa wa railimali za umma nchini.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, ameeleza hayo mjini Zanzibar wakati akisoma hotuba kwa niaba ya rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi alipomuwakilisha kwenye ufunguzi wa Jukwa la Mkutano wa Pili wa Sekta ya Umma na Wakaguzi wa Ndani Tanzania.

Makamu wa  kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman akipokea zawadi kutoka kwa rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa ndani Tanzania, Zelia Nyenza baada ya kufungua Jukwaa la Mkutano wa Tasisi za wakaguzi wa Tanzania.

Amesema, Tanzania inashuhudia mabadiliko makubwa kutokana na msukumo wa jamii, na kulazimika kuongezeka uwazi katika matumizi ya fedha za umma na kwamba hatua hiyo inahitaji Kamati, Bodi, Maafisa Masuuli na Wakaguzi wa ndani kujipanga vyema ili kuwezesha mageuzi kwenye muelekeo wa ufikishaji huduma katika kuenua maisha ya watu nchini.

Mkutano huo utatoa fursa kwa wadau wa Ukaguzi na Utawala kubadilishana mawazo na uzoefu juu yambinu bora zitakazosaidia kuleta mageuzi ya kiutawala kwenye taasisi zote za umma na binafasi na kutoa muono wa mbinu na mikakati sahihi yakufikia lengo la mageuzi kwenye sekta ya umma kwa maslahi ya wananchi.

Tukitaka maendeleo Katiba mpya haikwepeki - CHADEMA
Robertinho aahidi kuishangaza Afrika