Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteuwa Mhandisi Rogatus Mativila kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Miundombinu) na Mhandisi Mohamed Besta kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania – TANROADS.
