Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Sixtus Mapunda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa.

Mapunda anachukua nafasi ya Jane Nyamsenda ambaye uteuzi wake umetenguliwa na kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, imeeleza kuwa huo unaanza mara moja.
