Serikali Mkoani Mtwara, imesema takriban, wasichana 8,000 (miaka 10 – 19) wamepata ujauzito (kuanzia Januari – Disemba, 2022), huku zaidi ya asilimia 19.4 ya wajawazito wanaopata huduma katika vituo vya afya mkoani humo, wakiwa ni watoto wa chini ya umri wa miaka 19.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas katika Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Wilayani Tandahimba, na kuongeza kuwa takwimu hizo zinatokana na mfumo wa taarifa na upashaji habari za afya za mkoa.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas.

Amesema, ‘’mtoto wa kike bado anapitia vikwazo vinavyoweza kukwamisha kupata elimu na pengine hata kukatisha masomo yake kwani miongoni mwa vikwazo hivyo ni pamoja na mimba za utotoni na tatizo hili ni kubwa.”

Kufuatia hatua hiyo, ametoa wito kwa Jamii, taasisi zisizo za Kiserikali na Wadau wote kushirikiana na Serikali kupambana na ndoa, mimba za utotoni na vitendo vya ukatili, ili kuweza kufikia malengo ya kumkomba mtoto wa kike, kumuweka katika mazingira salama ya kumwezesha kufikia ndoto zake.

Ujenzi Daraja la JPM Kigogo - Busisi wafikia asilimia 70
Majina ya waliofariki ajali ya Basi Katavi yatajwa