Majina ya watu saba kati ya tisa waliofariki katika ajali ya basi la Komba’s iliyotokea katika mlima Nkondwe uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi yametajwa na Mganga Mkuu Wilaya ya Tanganyika, Dk Alex Mrema.

Mjina ya marehemu hao ni pamoja na Beka Mashaka (8), Edigar Gilidas (1.5), Anisia Kapandila (52), Toa Nzikwi (30), Eva Sylvanus (40), Eliud Mashaka (10), na Anthonia Kapandila (27), huku miili ya marehemu wawili ikiwa haijatambuliwa.

Eneo la ajali mara baada ya basi hilo kutumbukia mita 75 katika maporomoko na kuuwa watu saba.

Katika ajali hiyo, watu wengine 30 walijeruhiwa huku Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Ali Makame akisema chanzo cha ajali hiyo ni kufeli kwa breki na kusababisha basi hilo kukosa mwelekeo na kuporomoka bondeni.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko alisema serikali imeguswa na ajali hiyo na akatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa waliopoteza maisha, huku akisisitiza madereva kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani.

Takwimu: Wasichana 8,000 wapata ujauzito Mtwara
Urasimu, dhuluma waivunja Kamati Mipango miji Mwanza