Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Balozi wa Uswisi hapa nchini ambaye pia ni Mkuu wa Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano wa Kimataifa, Leo Näscher kuhusu ushirikiano katika eneo la Utamaduni na Sanaa baina ya nchi hizo mbili.

Kikao hicho kimefanyika hii leo Machi 9, 2023 katika ofisi za Wizara hiyo yenye Makao yake Makuu katika Mji wa Serikali Mtumba uliopo jijini Dodoma.

Leo Näscher, Naibu Balozi wa Uswisi hapa nchini ambaye pia ni Mkuu wa Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano wa Kimataifa (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao na Bw. Saidi Yakubu, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo (kulia) Machi 9, 2023 katika ofisi za Wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma.

Amesema, azma ya Serikali ni kusimamia sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo ambazo zinatoa ajira kwa vijana wengi na zina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi na namna watakavyoshirikiana katika kubadilishana utaalam na uzoefu katika sekta hizo.

Kwa upande wake Leo Näscher, Naibu Balozi wa Uswisi hapa nchini ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano wa Kimataifa amesema wana Jukwaa la Maendeleo ya Sekta ya Utamaduni – DGP litaendelea kushirikiana na Wizara kama kiunganishi cha wadau mbalimbali wa sekta za Utamaduni na Sanaa wakisaidia kiutaalam na ushauri.

Sangoma asalimisha Watoto wake 12 kupata chanjo ya Surua
GGML Ladies watoa vifaa tiba kwa akina mama Wajawazito