Lydia Mollel – Morogoro.

Katika kuhakikisha matumizi ya mkaa na kuni yanapungua Nchini, Wanawake Wajasiriamali 200 wamekabidhiwa majiko ya Gesi ili kulinda na kuboresha mazingira kwa lengo la kuepusha majanga ambayo huenda yanaweza kutokea kutokana uharibifu wa mazingira.

Zoezi hilo limefanywa Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro, Salim Alaudin Hasham katika viwanja vya ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga ambapo amekabidhi majiko hayo 200 kwa wanawake wajasiriamali ili kuwainua kiuchumi kupitia kazi zao kwa Mama lishe 200.

Kwa upande wa Mama lishe hao wamemshukuru Mbunge kwa kuwatambua na kuwakumbuka kwani kuwapatia majiko hayo yatawasaidia katika shughuli zao na wamemuomba kuendelea kuwakumbuka mara kwa mara ili kuwasikiliza na kutatua kero zao.

Wakurugenzi, Mameneja TANESCO kemeeni rushwa - Dkt. Biteko
Makala: Shamba la utafiti wa Wafu