Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema nchi yake haitaweza kustahamili ongezeko lingine la wahamiaji wanaowasili kutoka Afghanistan.
Kwa mujibu wa Idhaa ya kiswahili DW wakizungumza kwa njia ya simu na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani, na Rais Erdogan amesema wimbi jipya la wahamiaji halikwepeki iwepo hakuna hatua madhubuti zitakazochukuliwa nchini Afghanistan na Iran.
Erdogan amemweleza kansela Merkel kuwa Uturuki ambayo tayari inawahifadhi wakimbizi milioni 5 haitaweza kupokea ziada ya wahamiaji. Kwenye mazungumzo hayo bibi Merkel amesema kipaumble cha serikali yake kwa sasa ni kuwahamisha watu kutoka Afghanistan.
Erdogan anaulaumu Umoja wa Ulaya kwa kukwepa pendekezo la Uturuki la kuufanyia marekebisho mkataba baina yao wa mwaka 2016 ulionuwia kudhibiti wimbi la wahamiaji kwenye mataifa ya Ulaya kwa kuipatia fedha nchini yake ili kuwapatia hifadhi.