Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amewataka wadau wa sekta ya Utalii nchini kuungana na Serikali katika vita dhidi ya ujangili pamoja na uvamizi wa maeneo yaliyohifadhiwa baadala ya kuiachia Serikali pekee
Ametoa kauli hiyo mkoani Ruvuma mara baada ya kufanya doria kwa kutumia ndege ndogo katika maeneo yaliyohifadhiwa na kujionea uharibifu mkubwa unaoendelea kufanywa na wavamizi wakiwemo wakulima na wafugaji.
Amewataja wadau hao kuwa ni Chama cha Wasafirishaji wa Watalii ( TATO), Chama cha Mahotelia ( HAT) Chama cha Wawindaji wa Kitalii ( TAHOA) Shirikisho la Vyama vya Utalii nchini ( TCT ) pamoja Chama cha Waongoza Wataii ( TTGA)
Dkt.Ndumbaro amesema kutokana na kasi ya Wafugaji kuingiza mifugo na Wakulima kuendelea kulima ndani ya maeneo ya Hifadhi kunatishia kupungua au kuisha kabisa kwa Wanyamapori ambao watalii hutoa pesa nyingi kuja nchini kwa ajili ya kuwaona.
Kwa mujibu wa takwimu, sekta ya Utalii nchini inategemea zaidi ya asilimia 80 ya utalii wa wanyamapori.