Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kigoma Mjini Jana, March 25, 2023 walifanya Usafi katika fukwe za ziwa Tanganyika Zilizopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji.

Usafi huo, umefanyika ikiwa ni katika kuunga juhudi ya Serikali katika kampeni ya ‘Fukwe safi -Ziwa Salama” yenye lengo la kusafisha na kuondoa taka katika fukwe mbalimbali katika maziwa Mkuu ikiwemo ziwa Tanganyika, Victoria na Ziwa Nyasa

Utupaji wa taka ovyo, hasa za plastiki ziwani ambazo haziozi na badala yake huvunjika katika vipande vidogo ambavyo huweza kuleta athari kwenye mazalia ya Samaki na Samaki.
